Biblia inasema, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).
Yesu alisema, “mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” — maisha kamili yenye kusudi (Yohana 10:10).
2. Kutenganishwa
Sisi ni wenye dhambi na tumetenganishwa na Mungu.
Sote tumefanya, kufikiria au kusema mambo mabaya, ambayo Biblia huita “dhambi.” Biblia inasema, ” kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 03:23).
Mshahara wa dhambi ni mauti, utenganisho wa kiroho na Mungu (Warumi 6:23).
3. Yesu
Mungu alimtuma Yesu kufa kwa ajili ya dhambi zako.
Hii ni habari njema.
Yesu alikufa kwa ajili yetu ili tuweze kuwa na uhusiano na Mungu na kuwa pamoja Naye milele.
“Mungu Onyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu” (Warumi 5:8).
Lakini haikukoma alipokufa msalabani. Alifufuka tena na bado anaishi!
“Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu… Akazikwa… Akafufuka siku ya tatu, kulingana na Maandiko” (1 Wakorintho 15:3-4).
Yesu ndiye njia ya pekee ya kumfikia Mungu
Yesu alisema:, “Mimi ni njia, na ukweli na uhai; hakuna mtu awezaye kuenda kwa Baba, ila kupitia kwangu” (Yohana 14:6).
4. Omba
Omba ili upate msamaha wa Mungu.
Kuomba ni kuzungumza na Mungu tu. Anakujua. Kilicho muhimu ni mtazamo wa moyo na uaminifu wako. Omba sala kama hii ili umkubali Yesu kama Mwokozi wako:
“Yesu Kristo,
naomba msamaha kwa mambo mabaya niliyoyafanya katika maisha yangu. Asante kwa kufa Msalabani kwa ajili yangu, niweke huru kutoka kwa dhambi zangu zote na unisamehe leo. Tafadhali ingia maishani mwangu na unijaze na Roho wako Mtakatifu. Ishi nami milele.
Asante Yesu!”
Pata maelezo zaidi kuhusu Yesu Kristo.
Ni wa siri kwa asilimia 100%